Copyright by Tanzania Kids (2015). Powered by Blogger.
Thursday, 30 April 2015
MJENGEE MTOTO WAKO HALI YA KUJIAMINI…
Kujiamini
ni kama silaha ya mtoto dhidi ya changamoto za dunia. Watoto wanao jiamini hujisikia vizuri. Mara nyingi huwa na furaha na kufurahia maisha.
Kwa upande
mwingine, watoto wasiojiamini wanapata changamoto nyingi; kubwa zaidi ni kuwa na
wasiwasi mara kwa mara.
Mtoto
ambaye ana furaha na anafanya
vizuri katika masomo na michezo lakini hapati upendo hali hii inapunguza
uwezo wake wa kujiamini.
Mara
baada ya watoto kufikia utu uzima, ni vigumu kufanya mabadiliko ya kitabia
yanayochangia kujiamini kwao; woga huendelea kujengeka hivyo kushindwa
kujiamini .
Tuwape
moyo watoto katika kujaribu, wakishindwa, kujaribu tena, wajaribu tena, na
hatimaye kufanikiwa; hivyo wao wenyewe wataanza kufahamu kuhusu uwezo wao.
Wazazi,
walezi , walimu na jamii kwa ujumla wanaweza kukuza uwezo wa kujiamini kwa
watoto kwa kuwapa moyo.Kuepuka kulenga eneo moja maalum, kwa mfano, mafanikio
katika mtihani; ambayo yanaweza kusababisha watoto kuwa na hisia kwamba wao ni muhimu tu kama watafaulu mitihani.
Jinsi wazazi
Wanavyoweza kutoa msaada kwa watoto
Jinsi
gani wazazi wanaweza kutoa msaada wa kukuza afya, kujithamini na kujiamini kwa
mtoto?
• Kuwa
makini nini wanasema kwa watoto wao
Kumbuka kuwasifu mtoto wako si tu kwa kazi nzuri,
lakini pia kwa juhudi
• Kuwa
mfano wa kuigwa
• Kuwa
na hiari na upendo
Upendo
wako utasaidia kuongeza kujithamini kwa mtoto wako. Kuwakumbatia watoto na
kuwaambia watoto unawapenda kunasaidia kuweka juhudi kuelekea kitu au kujaribu
kitu ambacho awali alishindwa.
•
Kutoa maoni sahihi
Hii itafanya
watoto kujenga uthubutu.Pia inaonyesha unatambua
hisia ya mtoto na kumpa moyo kufanya uchaguzi sahihi tena wakati mwingine.
•
Kujenga usalama na upendo kwenye mazingira ya nyumbani
Watoto
ambao hawana usalama au wananyanyaswa
nyumbani hushindwa kujiamini.
• Kuwasaidia
watoto kuwa kutumia uzoefu uliopita kufanikisha shughuli mpya kwa kujiamini
No comments:
Post a Comment